1: KUPIGA
MSWAKI:
- · Piga mswaki kwa daikika 2 angalau mara mbili kwa siku.
- · Ni nyema kupiga mswaki kabla ya kulala kwani ulinzi wa meno kwa mate yako ni mdogo ukilinganisha na uwapo macho.
- · Kupiga mswaki baada ya kula ni mazoea mazuri, hukinga uchafu utoknao na chembe za chakula kujijenga kati kati ya meno yako.
2: KUTUMIA
‘MOUTH WASH’:
- · Tafuta na tumia ‘Mouth Wash’ uipendayo kuyapa nguvu meno yako.
- · Soma maelekezo kan-bla ya matumizi.
- · Wafundishe watoto kati ya miaka 6 -12 jinsi inavyotumiwa ili wasiimeze.
- · Kumbuka ‘Mouth wash ’ haimezwi.
3: UCHAGUZI
WA VYAKULA SAHIHI:
- · Chagua vyakula vyako kwa makini.
- · Epuka kula kula ovyo, jambo linaloongeza uchafu utokanao na vyakula kwenye meno.
- · Epuka vyakula vyenye sukari na vinavyonata, vyakula vya aina hii utengeneza mazingira ya bakteria kuzaliana kwa winigi mdomoni.
- · Pata mlo sahihi (Balance diet ) kwa ulinzi wa meno yako. Mfano ni maji mengi, mboga mboga, matunda, maziwa nk.
4: KUONANA NA DAKTARI WA MENO:
Jenga
tabia ya kuonana na tabibu wa meno angalau mara moja kwa miezi sita na kila
uhisapo maumivu ya meno kwa ajili ya utafiti na usafi wa meno yako.